Alibainisha kwamba: "Wanawake wa Kiislamu wanayo nafasi muhimu sana katika kusambaza ujumbe wa Imam Hussein (a.s). Katika tukio la Karbala, Wanawake kwa ushiriki wao wa moja kwa moja na kwa kustahimili mateso na majonzi, waliufikisha ulimwenguni ujumbe wa dhulma aliyoipata Imam Hussein (a.s) na msimamo wake wa Haki". Alitoa mfano kwa Bi. Zainab (sa) akisema: "Nafasi ya Bibi Zainab (s.a) kama Mwanamke na kama msemaji mkuu wa tukio la Karbala na mjumbe mashuhuri wa ujumbe wa A'shura, ni ya kipekee na haina mfano".
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Hojjatul - Islam wal Muslimina, Dr. Ali Taqavi, Rais wa Jamiat Al-Mustafa (s) - Tanzania, Leo hii (Tarehe 3, Julai, 2025), amehudhuria katika Madrasa ya Mabanati wa Kiislamu ya Hazrat Zainab (s) iliyopo chini ya Jamiat al-Mustafa (s) - Kigamboni, Dar-es-Salaam, Tanzania, na kuzungumza na Wanafunzi wa Madrasa hii katika muktadha wa Maombolezo ya Shahada ya Imam Hussein (as), akiwahimiza kuwaiga Wanawake wa Ahlul-Bayt (as) katika Njia ya kuendeleza Uislamu, kuhifadhi na kuitangaza wazi wazi Historia sahihi ya Karbala.
Katika mada yake, alizungumzia Umuhimu wa Mwanamke wa Kiislamu katika kufikisha Ujumbe wa Kiislamu katika Jamii ya Mwanadamu, na alisema:
Wanawake wa Kiislamu wanayo nafasi muhimu sana katika kusambaza ujumbe wa Imam Hussein (a.s). Katika tukio la Karbala, Wanawake kwa ushiriki wao wa moja kwa moja na kwa kustahimili mateso na majonzi, waliufikisha ulimwenguni ujumbe wa dhulma aliyoipata Imam Hussein (a.s) na msimamo wake wa Haki.
Alitoa mfano kwa Bi. Zainab (sa) akisema: "Nafasi ya Bibi Zainab (s.a) kama Mwanamke na kama msemaji mkuu wa tukio la Karbala na mjumbe mashuhuri wa ujumbe wa A'shura, ni ya kipekee na haina mfano".
Mbali naye, Wanawake wengine kama vile Ummu Kulthum (s.a) na Wanawake wengine wa Ahlul Bayt (a.s) pia walishiriki kwa namna ya kipekee katika kutangaza na kueneza ujumbe huo mtukufu.
Wanawake hawa, kwa kustahimili mateso na majonzi ya Karbala, waliwasilisha ujumbe wa msimamo na upinzani dhidi ya dhulma. Kupitia machozi yao na vilio vyao vya huzuni, waliamsha hisia za watu na kueneza ujumbe wa haki, uvumilivu, na ujasiri kwa vizazi vyote.
Wanawake wengine kama vile: Mke wa Muslim bin Aqil (ra), Ummu Wahab, na Mama wa Mashahidi wa Karbala, walichukua nafasi muhimu katika kumuunga mkono Imam Hussein (a.s) na wafuasi wake. Kwa kuonyesha kujitolea kwao na ushujaa wa wapendwa wao, walichangia pakubwa katika kusambaza ujumbe wa Imam Hussein (a.s) na kusimamia haki mbele ya dhulma.
Nafasi ya Wanawake katika kuhifadhi Ujumbe na Historia ya Kiislamu:
Kihistoria, Wanawake walikuwa na mchango mkubwa katika kuhifadhi na kusambaza simulizi (Historia) na kumbukumbu za tukio la A'shura. Kupitia juhudi zao, ujumbe wa Imam Hussein (a.s) uliweza kufika kwa vizazi vijavyo bila kupotoshwa.
Kwa ujumla, wanawake wa Kiislamu, katika tukio la A'shura na katika historia yote ya Kiislamu, kwa mchango wao katika nyanja mbalimbali, wameeneza ujumbe muhimu kwa dunia nzima - ikiwemo pamoja na kusimama dhidi ya dhulma, kutetea wanaodhulumiwa, na kulinda maadili ya Kiislamu.
Alisisitiza kwamba: Wanawake wote wa Kiislamu (hususan wapenzi na wafuasi halisi wa Mtume Muhammad s.a.w.w na Ahlul-Bayt wake watoharifu, amani iwe juu yao), hivyo ndivyo wanavyopaswa kuwa daima katika Maisha yao, kwa kuwaiga Wanawake wa Ahlul-Bayt (as) waliopigania Uislamu katika maisha yao yote, na kuishi Maisha yao kwa heshima na Utukufu mkubwa wakifuata na kushikamana kikamilifu na misingi bora na maadili safi ya Kiislamu.
Your Comment